Soma Kabla ya Kuagiza
Maelezo haya ni muhimu — soma kwa makini kabla ya kuchagua kifurushi na kutuma orodha ya wageni.
Soma vizuri maelezo ya kila kifurushi (Basic/Standard/Premium) kabla ya kuagiza, ili uchague kinachofaa tukio lako.
Hakiki MAJINA na NAMBA ZA SIMU za wageni wote kabla ya kutuma orodha. Ujumbe ukiwa umetumwa (hata kama jina/namba si sahihi), inahesabika kama kadi limetumika — halirejeshwi bure.
Wakati wa kuorodhesha wageni, tofautisha wazi kati ya “Single” (mgeni mmoja) na “Double” (wanandoa/familia — watu wawili) — hii inaathiri jinsi mwaliko unavyowekwa kwa jina.
Marekebisho ya bure ni MARA MOJA tu kwa kila design — mabadiliko ya ziada yanaweza kuwa na gharama ndogo ya ziada.
Taarifa za tukio (tarehe, mahali) zikibadilika BAADA ya kuthibitishwa, tuarifu HARAKA ili kurekebisha ratiba ya “Save the Date”/ukumbusho (Standard & Premium).
NIVLE Designs · Mialiko ya Kidigitali yenye Mtindo